Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 19

Luka 19:22-37

Help us?
Click on verse(s) to share them!
22Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda.
23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?
24Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.'
25Wakamwambia, `Bwana, yeye ana mafungu kumi.'
26'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
27Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu.”
28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
29Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
30akisema: `Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.
31Kama mtu akiwauliza, `Mbona mnamfungua?' Semeni, “Bwana anamhitaji.”
32Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.
33Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, 'Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?'
34Wakasema, `Bwana anamhitaji.'
35Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.
36Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.
37Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,

Read Luka 19Luka 19
Compare Luka 19:22-37Luka 19:22-37