Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 18

Luka 18:20-35

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Unazijua amri: Usizini; usiue; usiibe; usitoe ushahidi wa uongo; waheshimu baba yako na mama yako.”
21Yeye akasema, “Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu.”
22Yesu aliposikia hayo akamwambia, “Unatakiwa bado kufanya kitu kimoja: uza kila ulicho nacho, wagawie maskini, na hivyo utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate.”
23Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu alikuwa tajiri sana.
24Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!
25Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
26Wale watu waliposikia hayo, wakasema, “Nani basi, atakayeokolewa?”
27Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa Mungu.”
28Naye Petro akamwuliza, “Na sisi je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!”
29Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba au mke au kaka au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
30atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na kupokea uzima wa milele wakati ujao.”
31Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
32Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya na kumtemea mate.
33Watampiga mijeledi, watamuua; lakini siku ya tatu atafufuka.”
34Lakini wao hawakuelewa hata kidogo jambo hilo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
35Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba.

Read Luka 18Luka 18
Compare Luka 18:20-35Luka 18:20-35