Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 14

Luka 14:19-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
19Na mwingine akasema, `'Nimenunua jozi tano za ng'ombe, na mimi naenda kuwajaribu. Tafadhali uniwie radhi.'
20Na mtu mwingine akasema, 'Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.'
21Mtumishi akarudi na kumwambia bwana wake mambo hayo. Yule mwenye nyumba alikasirika akamwambia mtumishi wake, `'Nenda upesi mitaani na katika vichochoro vya mji ukawalete hapa maskini, vilema, vipofu na walemavu.”
22Mtumimishi akasema, `Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa bado kuna nafasi.'
23Bwana akamwambia mtumishi, 'Nenda katika njia kuu na vichochoro na uwashurutishe watu waingie, ili nyumba yangu ijae.
24Kwamaana nawaambia, katika wale walioalikwa wa kwanza hapana atakayeonja sherehe yangu.'
25Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia,
26'Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo?

Read Luka 14Luka 14
Compare Luka 14:19-28Luka 14:19-28