Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 12

Luka 12:3-52

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba.
4Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya,
5Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo.
6Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu.
7Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.
8Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
9Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu.
10Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.
11Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema,
12kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
13Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.”
14Yesu akamjibu, ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu.?
15Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”
16Yesu akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana,
17na akajiuliza ndani yake, akisema, nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu?
18Akasema, nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine.
19Nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.”
20Lakini Mungu akamwambia, ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?
21Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.
22Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu__ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu __ya kuwa mtavaa nini
23Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
24Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege!
25Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?
26Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?.
27Angalieni maua -yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,
28Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? enyi wa imani haba!
29Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu.
30Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.
31Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
32msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.
33Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa__hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
34Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
35Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,
36na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.
37Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.
38Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
39Zaidi ya hayo, mjue hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.
40Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.
41Petro akasema, “Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu.?
42Bwana akawaambia, “Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?
43Amebarikiwa mtumishi yule, ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya yale aliyoagizwa.
44Hakika nawaambia ninyi ya kuwa atamweka juu ya mali yake yote.
45Lakini Mtumishi yule akisema moyoni mwake, “bwana wangu anachelewa kurudi; hivyo akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, kisha akaanza kula, kunywa na kulewa,
46bwana wake yule mtumwa atakuja katika siku asiyotegemea na saa asiyoijua, naye atamkata vipande vipande na kumuweka katika sehemu pamoja na wasiokuwawaaminifu'
47Mtumishi, anayejua mapenzi ya bwana wake, naye hakujiandaaa wala hakufanya sawa sawa na mapenzi yake, atapigwa viboko vingi.
48Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi.
49Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka,
50Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika!
51Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko.
52Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu.

Read Luka 12Luka 12
Compare Luka 12:3-52Luka 12:3-52