Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya - Isaya 10

Isaya 10:20-33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Siku hiyo, mabaki ya Israeli, familia ya Yakobo ambayo imekimbia, hawatategemea kushindwa, lakini watamtegemea Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
21Mabaki ya Yakobo yatarudi kwa Mungu mwenye nguvu.
22Kwa kupitia watu wako, Israeli ni kama mchanga kama pwani ya bahari, Mabaki yao tu ndio yatakayorudi. Uaribifu wa amri, na mahitaji ya wingi wa haki.
23Maana Bwana wa majeshi, anakaribia kuleta uharibifu utachukua nafasi kubwa kitika nchi.
24Hivyo basi Bwana Yahwe wa majeshi anasema, ''watu wangu mhishio Sayuni, msiwaogope watu wa Asiria. Atawangamiza nyie kwa fimbo na atawanyua wafanyakazi juu yenu, kama ilivyotokea kwa Wamisri.
25Msimuogope, kwa mda mfupi hasira yangu itakwisha juu yenu, na hasira yangu italeta uharibifu.''
26Hivyo Yahwe wa majeshi atapiga mjeledi juu yenu kama vile alivyoishinda Midiani karibu na mwamba Orebu. Na atanyanyua fimbo yake juu ya bahari kama alivyofanya kule Misri.
27Siku hiyo mzigo wake utanyanyuliwa kwenye mabeba yako na nira katika shingo yako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya unene.
28Adui amekuja Aiathi na amepitia Migroni; katika Michmashi ameyahifadhi mahitaji yake.
29Wamevuka juu ya njia na wamepunzika huko Geba. Rama inatetemeka na Gibea ya Sauli imekimbia.
30Lia kwa sauti, ewe binti wa Galimu! sikiliza, Laishashi! Maskini Anathothi!
31Madmena ni mkimbizi na mkazi wa Gebuni wamejikusanya wanakimbia kutafuta msada.
32Siku hizi za leo atasimulia huko Nobi na atatingisha mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu.
33Tazama, Bwana Yahwe wa majeshi atapunguza matawi kwa nguvu za kutisha; miti mirefu itakatwa chini, wanaojivuna wataangushwa.

Read Isaya 10Isaya 10
Compare Isaya 10:20-33Isaya 10:20-33