Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 2

Hesabu 2:3-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Wale watakaopanga mashariki mwa hema ya kukutania, mahali ambapo juu huonekana wakati wa jua kuchomoza, ni makambi ya Yuda nao watakuwa katika kundi lao. Nashoni mwana wa Aminadabu ni kiongozi wa watu wa Yuda.
4Idadi ya watu wa Yuda ni 74, 600.
5Kabila la Isakari litapanga mbele ya Yuda. Nethaneli mwana wa Zuari ataliongoza jeshi la Isakari.
6Idadi ya kikosi chake ni wanaume 54, 000.
7Kabila la Zabuloni litapanga mbele ya Isakari. Eliabu mwana wa Heloni ndiye atakayeliongoza jeshi la Zabuloni.
8Idadi ya kikosi chake ni 57, 400.
9Idadi yote ya kambi y a Yuda ni 186, 400. Watakuwa wa kwanza kuondoka.
10Upande wa kusini kutakuwa na kambi ya Reubeni katika kundi lao. Kiongozi wa kundi la Reubeni ni Elizuri mwana wa Shedeuri.
11Idadi ya kikosi chake ni 46, 500.
12Simeoni atapanga mbele ya Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Zurishadai.
13Waliohesabiwa kwenye kikosi chake ni 59, 300.
14Kabila la Gadi litafuatia. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deuli.
15Idadi ya kikosi chake ni 45, 650.
16Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Reubeni, kulingana na kikosi chake, ni 151, 450. Watakuwa wa pili kuondoka.
17Kifuatacho, ni hema la kukutania kuondoka kambini pamoja na Walawi likiwa katikati ya kambi zote. Lazima waondoke hapo kambini kwa mpangilio huo kama walivyoingia kwenye kambi. Kila mwanamume lazima awe mahali pake kwa kufuata bango lake.
18Migawanyiko ya kambi y Efraimu kufuata mahali pake. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.
19Hesabu ya kikosi hiki ni 40, 500.
20Baada ya hao lilifuata kabila la Manase. Kiongozi wa Manase ni Gamaliel mwana wa Pedazuri.
21Hesabu ya kikosi hiki ni 32, 200.
22Kabila litakalofuata ni la Benjamini. Kiongozi wa Benjamini n Abidani mwana wa Gidioni.
23Hesabu ya kikosi hiki ni 35, 000
24Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu ni 108, 100. Watakuwa wa tatu kuondoka.
25Upande wa kaskazini kutakuwa na kambi ya kikosi cha Dani. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.

Read Hesabu 2Hesabu 2
Compare Hesabu 2:3-25Hesabu 2:3-25