Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 26

Hesabu 26:8-46

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Eliabu alikuwa mwana wa Palu.
9Wana wa Eliabu walikuwa ni Nemueli, Dathani. na Abiramu. Hawa ni walewale Dathani na Abiramu waliomfuata Kora waliompinga Musa na Haruni na kumpinga BWANA.
10Pale ambapo dunia ilifungua kinywa na kuwameza pamoja na Kora wakati ambapo wafuasi wa Kora walikufa. Wakati ule, moto uliteketeza wanaume 250, amboa wlikuwa ishara ya onyo.
11Lakini uzao wa Kora haukufa.
12Ukoo wa uzao wa Simeoni walikuwa hawa wafuatao: Kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli, kwa Jamini, ukoo wa Wajamini, kwa Jakini, ukoo wa Wajakini,
13kwa Zera, ukoo wa Wazera, kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14Hizi ndizo koo za uzao wa Simeoni, idadi yao ilikuwa wanaume 22, 200.
15Koo za uzao wa Gadi zilikuwa hizi: Kwa Zefoni, Ukoo wa Wazefoni, kwa Hagi, ukoo wa Wahagi, kwa Shuni, ukoo wa Washuni,
16kwa Ozini, ukoo wa Waozini, kwa Eri, ukoo wa Waeri,
17kwa Arodi, ukoo wa Waarodi, kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18Hizi ndizo koo za uzao wa Gadi, idadi yao walikuwa wanaume 40, 500.
19Wana wa Yuda walikwa Er na Onani, lakini hawa walifia katika nchi ya Kanaani.
20Koo zingine za uzao wa Yuda zilikuwa hizi: Kwa Shela, ukoo wa Washela, kwa Perezi, ukoo wa Waperezi, na kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21Uzao wa Perezi walikuwa hawa: Kwa Hezroni, ukoo wa Wahezroni, kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
22Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda, idadi yao ilikuwa wanaume 76, 500.
23Koo za uzao wa Isakari zilikuwa hizi: Kwa Tola, ukoo wa Watola, kwa Puva, ukoo wa Wapuva,
24kwa Jashubu, ukoo wa Wajashubu, kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
25Hizi ndizo zilikuwa koo za Isakari, Idadi yao ilikuwa wanaume 64, 300.
26Koo za uzao wa Zabuloni zilikuwa hizi: Kwa Seredi, ukoo wa Waseredi, kwa Eloni, ukoo wa Waeloni, kwa Jahaleeli, ukoo wa Wajahaleeli.
27Hizi ndizo zilikuwa koo za Zabuloni, idadi y ao ilikuwa wanaume 60, 500.
28Koo za uzao wa Ysufu zilikuwa Manase na Efraimu.
29Huu ndio uliokuwa uzao wa Manase: Kwa Machiri, ukoo wa Wamachiri (Machiri ndiye aliyekuwa baba wa Giliedi), kwa Giliedi, ukoo wa Wagiliedi.
30Wazo wa Giliedi walikuwa hawa wfuatao: Kwa Lezeri, ukoo wa Walezeri, kwa Helweki, ukoo wa Waheleki, kwa Asrieli,
31ukoo wa Asrieli wa Waasrieli, kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu,
32kwa Shemida, ukoo wa Washemida, kwa Hefa, ukoo wa Wahefa.
33Zelofehadi mwana wa Hefa hakuwa na watoto wa kiume bali alikuwa na mabinti. Majina ya binti zake yalikuwa Mahilahi, Noha, Hoglaha, Milika, na Tiriza.
34Hizi ndizo koo za Manase, idadi yao ilikuwa wanaume 52, 700.
35Koo za wana wa uzao wa Efraimu zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuthelaha, ukoo wa Washutheleha, kwa Becheri, ukoo wa Wabecheri, kwa Tahana, ukoo wa Watahana.
36Uzao wa Shuthelaha walikuwa, kwa Erani, ukoo wa Waerani.
37Hizi ndizo koo za uzao wa Efraimu, idadi yao ilikuwa wanaume 32, 500. Huu ndio uzao wa Yusufu, uliohesabiwa toka kila koo zao.
38Koo za uzao wa Benjamini zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Bela ukoo wa Wabela, kwa Ashibeli, ukoo wa Washibeli, kwa Ahiramu, ukoo wa Wahiramu,
39kwa Shefufamu, ukoo wa Washefumamu, kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.
40Wana wa Bela walikuwa ni Ardi na Naamani. Kutoka kwa Ardi ulijitokeza ukoo wa Waardi, na kutoka kwa Naamani ukajaitokeza ukoo wa Wanaamani.
41Hizi ndizo koo za uzao wa Benjamini. Idadai yao ilikuwa wanaume 45, 600.
42Kooo za uzao wa Dani zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo koo za uzao wa Dani.
43Idadi ya koo zote za Washuhamu ilikuwa wanaume 64, 400.
44Koo za uzao wa Asheri zilikuwa zifuatazo: Kwa Imna, ukoo wa Waimna, kwa Ishvi, ukoo wa Waishivi, kwa Beria, ukoo wa Waberia.
45Uzao wa Beria walikuwa hawa: Kwa Heberi, ukoo wa Waheberi, kwa Malikieli, ukoo wa Wamalikieli.
46Jina la binti wa Asheri lilikuwa Sera.

Read Hesabu 26Hesabu 26
Compare Hesabu 26:8-46Hesabu 26:8-46