Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 23

Hesabu 23:7-19

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Ndipo Balaamu alipoanza kunena unabii wake akisema, “Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka katika milima ya mashariki, 'Njoo, nilaanie Yakobo kwa ajili yangu,' alisema, 'Njoo umtie unajisi Israeli,'
8Nawezaje kuwalaani wale ambao Mungu hajawalaani? Nawezaje kuwapinga wale ambao Mungu hawapingi?
9Kwa kuwa kutoka juu ya miamba Ninamwona; kutoka kwenye milima ninamtazama. Kuna watu wanaoishi pekee yao na hawajioni wenyewe kama ni taifa la kawaida.
10Nani awezaye kuyahesabu mavumbi ya Yakobo au kuhesabu hata robo ya Israeli? Naomba nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wa maisha yangu uwe kama wake!”
11Balaki akamwambia Balaamu, “Umenifanyia nini? Nilikuleta ili uwalaani maadui wangu, lakini ona, umewabariki,”
12Balaamu akajibu akasema, “Kwa nini nisiwe mwangalifu kusema kile ambacho BWANA anaweka kinywani mwangu?”
13Basi Balaki akamwambia, “Hebu uje nami kwenye eneo jingine ili uwaone. Utakaowaona ni wale wa karibu tu, huwezi kuwaona wote. Huko sasa unaweza kunilaania hawa watu.”
14Kwa hiyo akampeleka Balaamu kwenye shamba la Zofimu, lililo juu ya Mlima Pisiga, na kule akajenga madhabau zingine saba. Akatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume kwa kila madhabahu.
15Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Simama hapa karibu na sadaka zako, wakati mimi naenda kukutana na BWANA kule.”
16Kwa hiyo BWANA akakutana na Balaamu na kumwekea ujumbe kinywani mwake. Alimwambia, “Rudi kwa Balaki ukamwambie huu ujumbe toka kwangu.”
17Balaamu akamrudia, na tazama, alikuwa amesimama karibu na sadaka zake za kuteketezwa, na vionigozi wa Moabu walikuwa pamoja naye. Balaki akamwuliza, “BWANA amekwambiaje?”
18Balaamu akaanza kutoa unabii. Akasema, “Inuka, Balaki na usikilize. Nisikilize mimi wewe mwana wa Zippori.
19Mungu siyo mtu, kwamba umdanganye, au mwanadamu awezaye kubadili mawazo. Je, alishawahi kuahidi kitu pasipo kukitekeleza? Je, alishawahi kusema kuwa atafanya kitu bila kufanya kama alivyosema?

Read Hesabu 23Hesabu 23
Compare Hesabu 23:7-19Hesabu 23:7-19