Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 22

Hesabu 22:8-19

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Balaamu akawaambia, “Bakini hapa usiku wa leo. Kesho nitawaletea atakachoniambia BWANA.” Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakabaki na Balaamu kwa usiku huo.
9Mungu akaja kwa Balaamu na kumwambia, “Ni akina nani hawa waliokuja kwako?”
10Balaamu akamjibu Mungu, “Balaki mwana wa Zippori, Mfalme wa Moabu amewatuma kwangu. Alisema,
11'Tazama hawa watu waliotoka Misri wanafunika uso wa nchi yangu. Sasa naomba uje unilaanie hawa watu. Labada nitaweza kuwa kuwashinda na kuwafukuza.'”
12Mungu akamjiu Balaam, “Usiambatane na hao wanaume. Na usiwalaani hawa wana wa Israeli kwa sababu wamebarikiwa.”
13Balaamu akaamka asubuhi na kuwaambia wale viongozi wa Balaki,. “Rudini nchini kwenu kwa sababu BWANA amenikataza kuambatana nanyi.”
14Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, “Balaamu amekataa kuambatana nasi.”
15Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali.
16Wakaja kwa Balaamu na kumwambia, “Balaki mwana wa Zippori anasema hivi, 'Tafadhali hebu kitu chochote kisikuzuie kuja kwangu,
17kwa sababu nitakulipa malipo mazuri sana na kukupa heshima kubwa, nami nitakufanyia chochote utakachoniambia. Tafadhali sana uje unilaanie hawa watu.'”
18Balaamu akawajibu watu wa Balaki akawaambia, “Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitaweza kufanya dhidi ya maneno ya BWANA, Mungu wangu na kufanya pungufu au zaidi ya kile anachoniambia.
19Sasa basi, tafadhali subirini hapa usiku wa leo pia, ili kwamba nipate kujifunza kitu zaidi ambacho BWANA ananiambia.”

Read Hesabu 22Hesabu 22
Compare Hesabu 22:8-19Hesabu 22:8-19