Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 22

Hesabu 22:26-33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
26Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine.
27Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake.
28Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, “Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?”
29Balaamu akamjibu yule punda, “Ni kwa sababu umenitendea kwa ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuwa nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua.”
30Yule punda akamwambia Balaamu, “Je, mimi si punda wako ambaye umenipanda maishani mwako mwote mpaka hivi sasa? Je, nimewahi kuwa na tabia ya kukufanyia hivi hapo awali?” Balaamu akasema “hapana.”
31Basi BWANA akafungua macho ya Balaamu, na akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Balaamu akainamisha kichwa chake chini.
32Yule malaika wa BWANA akamwambia, “Kwa nini umempiga punda wako mara tatu? Tazama, Nimekuja kama adui yako kwa sababu matendo yako kwangu yamekuwa maovu.
33Yule punda aliniona na akageuka kutoka kwangu mara tatu. Kama asingekuwa amegeuka kutoka kwangu, hakika ningekuwa nimekua na yeye kumwacha hai.

Read Hesabu 22Hesabu 22
Compare Hesabu 22:26-33Hesabu 22:26-33