Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 21

Hesabu 21:21-32

Help us?
Click on verse(s) to share them!
21Kisha Israeli akatuma wajumbe kwa Sihoni mfalme wa Waamori akisema,
22Tunaomba tupite katika nchi yako. hatutapita katika shamba au kwenye shamba la mizabibu. Hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita katika njia kuu ya mfalme mpaka tutakapopita mpaka wako.”
23Lakini mfalme Sihoni hakumruhusu Israeli kupita kwenye mpaka wao. Badala yake, Sihoni akakusanya jeshi lake lote na kumvamia Isreli huko jangwani. Akaja kwa Jahazi, ambapo alipigana dhidi ya Israeli.
24Israeli akalivamia jeshi la Sihoni na nchi ya upanga na kuchukua nchi yao kutoka Amon mpaka mto Jabboki, hadi kufikia nchi ya watu wa Amoni. Sasa mpaka wa watu wa Amoni ulikuwa umefungwa.
25Israeli akachukua miji yote ya Waamori na akaishi ndani yake, pamoja na Heshiboni na vijiji vyake wote.
26Heshiboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alipigana dhidi ya mfalme wa kwanza wa Moabu. Sihoni alikuwa ameteka ardhi yake yote toka mipaka yake mpaka mto wa Amoni.
27Hiyo ndiyo sababu wala ambao huongea kwa Mitahali husema, “Njoni Heshboni. Mji wa Sihoni ujengwe na kuimarishwa tena.
28Moto uliwaka toka Heshiboni, moto kutoka mji wa Sihoni ambao uliiteketeza Ari ya Moabu, na wenyeji wa miji ya juu ya Amoni.
29Ole wako, Moabu! umepotea, enyi watu wa Chemoshi. Amewafanya watu wake kuwa wakimbizi na binti zake kuwa wafungwa wa Sihoni mfalme wa Waamori.
30Lakini tumempiga Sihoni. Tumeiangsmiza Heshibon mpaka Diboni. Tumewaharibu wote mpaka Nofa, ambayo inafika mpaka Madeba.”
31Kwa hiyo Israeli akaanza kuishi katika nchi ya Waamori,
32Kisha Musa akatuma watu kwenda kuingalia Yaziri. Waliviteka vijiji vyake na kuwafukuza Waamori waliokuwa wakiishi humo.

Read Hesabu 21Hesabu 21
Compare Hesabu 21:21-32Hesabu 21:21-32