Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 21

Hesabu 21:1-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Aradi mfalme wa Wakanaani, aliyekuwa akiishi Negebu, aliposikia kuwa Israeli alikuwa akisafiri kwa kupitia barabara kuelekea Atharimu, akapigana dhidi ya Israeli na kujitwalia baadhi ya mateka.
2Israeli akaapa mbele ya BWANA akasema, “Kama utatupa ushindi dhidi ya hawa watu, ndipo tutakapoingamiza kabisa miji yao,”
3BWANA akaisikia sautiya Israeli na kuwapa ushindi dhidi ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. Mahali pale paliitwa Horima.
4Wakasafiri kutoka Mlima Hori kwa barabara kuelekea bahari ya shamu wakiizunguka nchi ya Edomu. Watu walikufa moyo kwa njia hiyo.
5Watu wakamnung'unikia Mungu na Musa: “Kwa nini umetutoa Misiri ili tufa katika jangwa hili? Hapa hakuna mikate, wala maji, na chakula hiki dhaifu kimetukinai.”
6Basi Mungu akatuma nyoka wa sumu kati yao. Wale nyoka wakawauma wale watu; watu wengi walikufa.
7Watu wakaenda kwa Musa wakamwambia, “Tumetenda dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu na wewe. Mwombe Mungu atuondolee hawa nyoka.” Kwa hiyo Musa akawaombea watu.
8BWANA akamwambia Musa, “Tengeneza nyoka na umweke kwenye nguzo. Na itakuwa kila anayeumwa, akimwangalia huyo nyoka atapona,”
9Kwa hiyo Musa akatengeneza nyoka wa shaba naye akamweka juu ya nguzo. Na kila mtu alipoumwa na nyoka na kumwangalia huyo nyoka alipona.
10Kisha watu wa Israeli wakasafiri na kisha kuweka kambi Obothi.
11Kisha wakasafiri kutoka pale na kuweka kambi Iye Abarimu katika jangwa linalokabili Moabu kuelekea upande wa mashariki.
12Kutoka pale wakasafiri na kuweka kambi katika bonde la Zeredi.
13Kutoka pale walisafiri na kuweka kambi kwenye upande mwingine wa mto Amoni, ambao ukubwa wake unaanzia kwenye mpaka wa Waamori. Mto wa Amoni ndio unaootengeneza mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
14Ndiyo maana imeandikwa katika gombo la Kitabu cha BWANA, “Wahebu katika Sufa, na bonde la Amoni,
15mtelemko wa bonde linaloelekea katika mji wa Ari na kuelekea kwenye mpaka wa Moabu,”
16Kutoka pale wakasafiri mpaka Beeri, hapo ndipo palipo na kisima ambacho Bwana alimwambia Musa, “Wakusanye watu kwa ajili yangu ili uwape maji,”
17Ndipo Israeli waipoimba wimbo huu: “enyi visima, yajazeni maji. Imbeni juu ya kisima hiki.
18Kisima ambacho viongozi wetu walichimba, kisima ambacho wenye hekima walichimba kwa fimbo ya kifalme na kwa fimbo ya kutembelea.” Kisha kutoka jangwani walitembea mpaka Matanaha.
19Kutoka Matanaha walisafiri mpaka Nathalieli, na kutoka Nathalieli mpaka Bamothi,
20na kutoka Bamothi hadi kwenye bonde la Moabu. Hapo ndipo kilele cha Mlima Piska kinapoonekana jangwani.
21Kisha Israeli akatuma wajumbe kwa Sihoni mfalme wa Waamori akisema,
22Tunaomba tupite katika nchi yako. hatutapita katika shamba au kwenye shamba la mizabibu. Hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita katika njia kuu ya mfalme mpaka tutakapopita mpaka wako.”
23Lakini mfalme Sihoni hakumruhusu Israeli kupita kwenye mpaka wao. Badala yake, Sihoni akakusanya jeshi lake lote na kumvamia Isreli huko jangwani. Akaja kwa Jahazi, ambapo alipigana dhidi ya Israeli.
24Israeli akalivamia jeshi la Sihoni na nchi ya upanga na kuchukua nchi yao kutoka Amon mpaka mto Jabboki, hadi kufikia nchi ya watu wa Amoni. Sasa mpaka wa watu wa Amoni ulikuwa umefungwa.

Read Hesabu 21Hesabu 21
Compare Hesabu 21:1-24Hesabu 21:1-24