Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 20

Hesabu 20:4-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Kwa nini umewaleta watu wa BWANA kufia katika jangwa hili, sisi na wanyama wetu?
5Kwa nini ulitutoa Misri na kutuleta katika eneo hili baya? Hapa hakuna nafaka, wala mitini, wala mizabibu, wala makomamanga. Na hakuna maji ya kunywa.”
6Basi Musa na Haruni wakatoweka mbele ya mkutano huo. Wakaenda kwenye hema ya kukutania wakalala kifudifudi. Ndipo pale utukufu wa Busara wa BWANA ukaonekana kwao.
7BWANA akanena na Musa, akamwambia,
8“Chukua fimbo yako na uwakusanye watu, wewe na Haruni ndugu yako. Uumbie huu mwamba mbele ya macho yao, na uumuru utoe maji. Nawe utawapa maji kutoka kwenye huu mwamba, nawe utawapa maji ya kunywa hao watu na wanyama wao.”
9Musa akachukua hiyo fimbo mbele ya BWANA, kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.
10Kisha Musa na Haruni wakawakusanya watu pamoja mbele ya ule mwamba. Ndipo Musa akawaambia, “Sasa sikilizeni, enyi wapinzani. Lazima tuwape maji kutoka kwenye huu mwamba?”
11Ndipo Musa akanyosha mkono wake na kuupiga ule mwamba mara mbili kwa fimbo yake, na maji mengi yakatoka. Wale watu wakanywa pamoja na wanyama wao.
12Kisha BWANA akamwambia Musa na Haruni, “Kwa kuwa hamkuniheshimu mimi na kuniamini mbele ya watu wa Israeli, hamtawaingiza hawa watu katika nchi niliyowaahidi.

Read Hesabu 20Hesabu 20
Compare Hesabu 20:4-12Hesabu 20:4-12