Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 20

Hesabu 20:1-6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa hiyo wana wa Israeli, na jamii yote ya watu, wakaenda katika jangwa la Sini katika mwezi wa kwanza; wakaa Kadeshi. Hapo ndipo Miriamu alipofia na kuzikwa.
2Huko hapakuwa na maji kwa ajili ya watu, kwa hiyo wakakusanyika kinyume na Musa na Haruni huko.
3Watu wakamlalamikia Musa. Wakasema, “Ilikuwa ni bora kama tungelikufa wakati Waisraeli wenzetu walipokufa mbele za BWANA.
4Kwa nini umewaleta watu wa BWANA kufia katika jangwa hili, sisi na wanyama wetu?
5Kwa nini ulitutoa Misri na kutuleta katika eneo hili baya? Hapa hakuna nafaka, wala mitini, wala mizabibu, wala makomamanga. Na hakuna maji ya kunywa.”
6Basi Musa na Haruni wakatoweka mbele ya mkutano huo. Wakaenda kwenye hema ya kukutania wakalala kifudifudi. Ndipo pale utukufu wa Busara wa BWANA ukaonekana kwao.

Read Hesabu 20Hesabu 20
Compare Hesabu 20:1-6Hesabu 20:1-6