Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 1

Hesabu 1:1-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu alimwambia Musa katika hema ya kukutania walipokuwa katika jangwa la Sinai. Hii ilitokea katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili miaka miwili baadaya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Mungu alisema,
2'fanya sensa ya wanaume wote wa Israel kutoka kila ukoo, katika familia za baba zao. Wahesabu kwa majina, wahesabu kila mume, kila mwanamume
3kuanzia umri a miaka ishirini na zaidi. Uwahesabu wote wanaoweza kupigana kama askari wa Israel. Wewe na Haruni mtaandika idadi ya wanaume katika makundi ya majeshi yao.
4Kila mwanamume kwa kila kabila, kichwa cha ukoo, lazima atumike na wewe kama kiongozi wa kabila.
5Haya ndiyo majina ya viongozi ambao watapigana pamoja na wewe: Kutoka kabila la Reubeni, Elizuri mwana wa Shedeuri;
6kutoka kabila la Simeoni, Shelumiel mwana wa Zurishadai
7Kutoka kabila la Yuda, Nashoni mwana wa Aminadabu;
8Ktoka kabila la Isakari, Nethaneli mwana wa Zuari;
9kutoka kabila Zebuluni, Eliabu mwana wa Heloni
10kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yusufu, Elishama mwana wa Ammihudi; kutoka kabila la Manase, Gamaliel mwan wa Pedazuri;
11kutoka kabila la Benjamini mwana wa Ysufu, Abidani mwan wa Gidion;
12Kutoka kabila la Dan, Ahizeri mwana wa Amishadai;
13kutoka kabila Asheri, Pagieli mwana wa Okirani;
14kutoka kabila la Gadi, Eliasafu mwana wa Deuli;
15na kutoka kabila la Naftali, Ahira mwana wa Enani.”
16Hawa ndio wanaume waliochaguliwa kutoka kwa watu. Waliongoza kabila za mababu zao. Walikuwa viongozi wa koo katika Israel.
17Musa na Haruni wakawachukua wale wanaume, waliokuwa wameandikwa kwa majina,
18na pamoja na wanaume hao waliwakusanya wanume wote katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Kisha kila mwanume wa miaka ishirini na zaidi alitambua babu zake. Alitakiwa kutaja koo na famila kutoka katika ukoo.

Read Hesabu 1Hesabu 1
Compare Hesabu 1:1-18Hesabu 1:1-18