Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 19

Hesabu 19:8-20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Yule aliyemchoma huyo ng'ombe mke atafua nguo zake kwa maji na kuoga majini. Naye atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile.
9Baadaye mtu aliyesafi atayakusanya hayo majivu ya ng'ombe huyo na kuyaweka nje ya kambi kwenye eneo safi. Majivu haya yatatunzwa kwa ajili ya jamii ya watu wa Israeli. Watayachanganya majivu na maji kwa ajili ya utakaso wa dhambi, kwa kuwa majivu yalitokana na sadaka ya dhambi.
10Yule aliyeyakusanya majivu ya ng'ombe huyo lazima afue mavazi yake. Atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile. Hii itakuwa sheria ya kudumu kwa watu wa Israeli na kwa wageni wanaoishi nao.
11Yeyote atakayegusa maiti ya mtu atakuwa najisi kwa siku saba.
12Mtu wa jinsi hiyo atajitakasa mwenyewe siku ya tatu na siku ya saba. Ndipo atakapokuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu, basi hatakuwa safi siku ya saba.
13Yeyote atakayegusa mtu aliyekufa, maiti ya mtu aliyekufa na hajajitakasa - mtu huyu anainajisi masikani ya BWANA. Mtu huyo ataondolewa kuwa miongoni mwa Waisraeli kwa sababu maji ya farakano hayakunyunyiziwa kwake. Atabaki najisi; na unajisi wake utabaki kwake.
14Hii ndiyo sheri ya mtu anayefia hemani. Kila mtu aingiaye hemani na kila mtu ambaye tayari yumo hemani atakuwa najisi kwa siku saba.
15Kila chombo ambacho hakina kifuniko kinanajisika.
16Vivyo hivyo, kwa mtu aliye nje ya hema ambaye atamgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga wowote, au mfupa wa mtu, au kaburi—mtu huyo atakuwa najisi kwa siku saba.
17Fanyeni hivi kwa mtu najisi: twaeni majivu ya sadaka ya dhaambi ya kuteketezwa na myacahanganye kwenye chombo chenye maji ya mto.
18Ndipo mtu aliye safi atachukua hisopo, na kutia katika hayo maji, na kunyunyizia juu ya hema, na katika vyombo vyote vilivyo hemani, na kwa watu waliokuwepo, na kwa yule aliyegusa ule mfupa, mtu aliyeuawa, maiti, au kaburi.
19Katika siku ya tatu na siku ya saba, yule mtu aliye msafi atamnyunyizia yule mtu asiyekuwa safi. Katika siku ya saba mtu najisi atajitakasa mwenyewe. Atazifua nguo zake na kuoga kwenye maji. Jioni yake atakuwa safi.
20Lakini yule atakayebaki najisi, anayekataa kujitakasa mwenyewe — huyo mtu ataondolewa kutoka kwenye jamii, kwa sababu amepanajisi patakatifu pa BWANA. Hajanyunyiziwa maji ya utakaso; atabaki najisi.

Read Hesabu 19Hesabu 19
Compare Hesabu 19:8-20Hesabu 19:8-20