Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 15

Hesabu 15:5-34

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Na tena mtatoa pamoja na sadaka ya kuteketezwa, au kwa sadaka ya divai robo ya hini ya sadaka ya vinywaji kwa kila mwanakondoo.
6Kama unatoa sadaka ya kondoo dume, utaandaa sadaka ya unga ya sehemu za kumi mbili za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na sehemu ya tatu ya hini ya divai.
7Kwa sadaka ya kinywaji, mtatoa sehemu ya tatu ya hini ya divai ambayo itatoa harufu nzuri kwa BWANA.
8Utakapoandaa fahari kwa ajiliy a sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya kutimiza kiapo, au sadaka ya amani kwa BWANA,
9Ndipo utakapotoa sadaka ya fahari pamoja na sadaka ya unga ya sehemu za kumi tatu za unga mwembamba uliochanganywa na nusu ya hini ya mafuta.
10Mtatoa sadaka ya kinywaji nusu ya hini ya divai, sadaka iloyotengenezwa kwa moto ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA.
11Itafanyika hivi kwa kila fahari, kwa kila kondoo dume, na kila mwanakondoo dume au mbuzi mchanga.
12Kila sdaka utakayoindaa na kuitoa itafanyika kama ilivyoanishwa hapa.
13Wazawa wote wa Israeli watafanya mambo haya kwa utaratibu huu, yeyote atakayeleta sadaka iliyotengenezwa kwa moto, ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA.
14Na kama kuna mgeni anayeishi kati yenu, au yeyote atakayeishi na watu wa vizazi vyenu vyote, lazima atengeneze sadaka iliytoengenezwa kwa moto, ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Atafanya kama mnavyofanya.
15Kutakuwa na sheria hiyo hiyo kwa watu wote na kwa mgeni anayeishi kati yenu, sheria ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Ninyi mlivyo, ndivyo atakavyokuwa mgeni aliyeishi kati yenu. Atafanya kama mnavyofanya mbele ya BWANA.
16Sheria na amri hiyohiyo ndiyo itakayotumika kwa mgeni anayeishi kati yenu.”
17Tena BWANA akanena na Musa, akasema,
18“Nena wana wa Israeli uwaambie, 'mtakapofika katika nchi ninayowapeleka,
19mtakapokula chakula kinachozalishwa katika nchi hiyo, mtatoa sadaka ya kunipendeza mimi.
20Kutoka kwenye mikate yenu ya kwanza mtatoa mkate wa kuinuliwa kama sadaka iliyoinuliwa kutoka mahali pa kupuria nafaka. Mtaiinua kwa jinsi hii.
21Watu wa uzao wako wote wtanitolea sadaka ya kuinuliwa kutoka kwenye unga wenu wa kwanza.
22Wakati mwingine mtafanya dhambi pasipo kukusudia, Kama hamtatii amri zote hizi ambazo nimemwambia Musa
23-kila kitu ambacho nimewaamuru kupitia Musa kuanzia siku ambayo nilianza kuwaamuru na kuendelea kwa watu wote wa uzao wako.
24Kwa swala la dhambi isiyokusudiwa ambayo watu wote hawaijui, basi watu wote watatoa fahari mchanga sadaka ya kuteketezwa ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Pamoja na haya yote, lazima itengenezwe sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji, kama ilivyoagaizwa katika amri, na beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
25Kuhani atafanya sadaka upatanisho kwa watu wote wa Israeli. Watasemehewa kwa sababu dhambi haikukusudiwa. Wametoa sadaka yao, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili yangu. Wameleta sadaka yao kwangu iliyotengenezwa kwa moto. Wameleta sadaka yao ya uovu mbele yangu kwa ajili ya kosa lao.
26Ndipo watu wote wa Israeli watasamehewa, pia wageni wote wanaoishi kati yao, kwa sababu watu wote walitenda dhambi pasipo kukusudia.
27Kama mtu atatenda dhambi bila kukusudia, atatoa mbuzi jike wa umri wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
28Naye kuhani atafanya upatanisho kwa BWANA kwa ajili ya mtu yule aliyefanya dhambi pasipo kukusudia. Yule mtu atasamehewa baada ya upatanisho kufanyika.
29Mtakuwa na sheria hiyohiyo kwa mtu yeyote anayefanya dhambi hiyo pasipo kukusudia, sheria hiyohiyo hata kwa mzawa wa Isreli na kwa wageni wanaoishi kati yao.
30Lakini mtu afanyaye chochote kwa KUkusudia, awe mzawa au mgeni, ananikufuru mimi. Huyo mtu ataondolewa kati ya watu wake.
31Kwa sababu atakuwa amedharau neno langu na amevunja neno amri yangu, mtu huyo ataondolewa kabisa. Dhambi yake itakuwa juu yake.'”
32Wakati wana wa Israeli walipokuwa katika jangwa, wakamuona mwanamume akikusanya kuni sikiu ya Sabato.
33Wale waliomwona wakamleta kwa Musa, Haruni na kwa watu wote.
34Wakamweka kifungoni kwa sababu ilikuwa haijaamuliwa atakachotendewa.

Read Hesabu 15Hesabu 15
Compare Hesabu 15:5-34Hesabu 15:5-34