Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 14

Hesabu 14:12-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Nitawapiga kwa mapigo, na kuwaondolea urithi, na kufanya taifa kubwa kutoka kwenye ukoo wako ambalo litakuwa kubwa na lenye nguvu kuliko wao.
13Musa akamwambia BWANA, “Kama utafanya hivi, Na Wamisiri wakisikia habari hizi, na kwa sababu uliwaokoa kutoka kwao kwa nguvu zako.
14Basi watawaambia wakazi wa nchi hii. Wamesikia ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa, kwa sababu uso wako waonekana. Wingu lako husimama juu ya watu wetu. Wewe huwatangulia katika nguzo ya wingu wakati wa mchana na katika nguzo ya moto wakati wa usiku.
15Sasa kama utawaua hawa watu kama mtu mmoja, basi mataifa ambao wamesikia sifa zako watasema,
16“Kwa Sababu BWANA hana uwezo wa kuwapeleka watu hawa katika nchi ambayo aliwaapia kuwapa, ndiyo maana amewaua katika jangwa hili.'
17Sasa, nakusihi, utumie uweza wako. Kwa kuwa umesema kuwa,
18'BWANA si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa uaminifu katika agano. Yeye husamehe uovu na uasi. Kwa vyovyote vile atafutilia hatia atakapoleta hukumu ya dhambi za mababu juu ya wazao wao, kwa kizazi cha tatu na cha nne.'
19Ninakusihi uwasameha watu hawa dhambi zao kwa sababu ya ukuu wa uaminifu wa agano lako, kama vile ambavyo umekuwa ukiwasamehe watu hawa tokea wakati wakiwa Misri mpaka sasa.”
20BWANA akasema, Nimewasamehe kwa kama ulivyoomba,
21bali kama Niishivyo, na kama vile dunia yote itakavyojazwa na utukufu wangu,
22watu wote walioona utukufu wangu na ishara za nguvu zangu nilizotenda kule Misri na kule jangwani - Lakini bado wamenijaribu mara kumi sasa na hawakuisikiliza sauti yangu.
23Kwa hiyo nasema kwamba hakika hawataiona nchi ile ambayo niliwaahdi kuwapa mababu zao. Hakuna hata mmoja wao ambao wamenidharau watakaoiona,
24isipokuwa mtumishi wangu Kalebu, kwa sababu alikuwa na roho nyingine. Yeye amenifuata kwa ukamilifu; Yeye nitampeleka katika nchi hiyo ambayo alienda kuipeleleza. Wazao wake wataimilki.
25(Sasa Waamaleki na Wakanani waliishi katika bonde.) Kesho mtageuka na kwenda katika jangwa kwa njia ya bahari ya Shamu.”
26BWANA akanena na Musa na Haruni, akasema,
27“Nitaivumilia jamii ya watu hawa waovu ambao wananinung'unikia mpaka lini? Nimeyasikia malalamiko ya wana wa Israeli dhidi yangu.
28Waambie, 'Kama niishivyo,' asema BWANA, 'kama vile mlivyosema katika masikio yake, nitawafanyia jambo hili:

Read Hesabu 14Hesabu 14
Compare Hesabu 14:12-28Hesabu 14:12-28