Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme - 2 Wafalme 12

2 Wafalme 12:14-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Waliwapa hizi fedha wale ambao waliokuwa wamefanya kazi ya kutengeneza nyumba ya Yahwe.
15Pia, hakukuhitajika zile pesa zilipwe kwa ajili ya matengenezo ili kuwajibika kwa kuwa watu walizipokea nakuzilipa kwa watenda kazi, kwa sababu hawa watu walikuwa waadilifu.
16Lakini pesa kwa ajili ya matoleo ya hatia na pesa kwa ajili ya matoleo ya dhambi hazikuwa zimeletwa kwenye hekalu la Yahwe, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani.
17Kisha Hazaeli mfalme wa Shamu akashambuliwa na kupigana dhidi ya Gathi, na kuichukua.
18Ndipo Hazaeli akageuka kuishambulia Yerusalemu. Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vitu vyote ambavyo Yehoshefati na Yehoramu na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, na kuviweka wakfu, na vile alivyokuwa ameviweka wakfu, na dhahabu zote zilizokuwa zimeonekana kwenye gala la nyumba ya Yahwe na la mfalme akawatuma kwenda kwa Ahazi mfalme wa Shamu. Kisha Hazaeli akaenda zake kutoka Yerusamu.
19Kama mambo mengine yanayomuhusu Yoashi, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
20Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila.
21Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.

Read 2 Wafalme 122 Wafalme 12
Compare 2 Wafalme 12:14-212 Wafalme 12:14-21