Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 22

1Wafalme 22:33-53

Help us?
Click on verse(s) to share them!
33Ikawa majemedari wa magari walipoona kuwa yeye hakuwa mfalme wa Israeli, wakamwacha.
34Lakini mtu mmoja akavuta upinde wake kwa kubahatisha na akampiga mfalme wa Israeli katikati ya mwunganiko wa mavazi yake ya chuma. Ahabu akamawambia dereva wa gari lake, “geuza unirudishe kutoka vitani, kwa kuwa nimeumizwa sana.”
35Vita ikawa mbaya sana siku hiyo na mfalme akalazwazwa garini mwake akiwakabili Washami. Akafa jioni hiyo. Damu ilimwagika kutoka kwenye jeraha lake ndani ya gari.
36Ikawa wakati wa kuzama jua, kilio kikatawala kwa jeshi lote, wakisema, “Kila mtu arudi kwenye mji wake; na kila mtu arudi kwenye mkoa wake!”
37Kwa hiyo mfalme Ahabu akafa na akaletwa Samaria, wakamzika huko Samaria.
38Wakaliosha lile gari kwenye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake (hapa ni mahali ambapo makahaba waliogea), kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limesema.
39Kwa mambo mengine yanayohusisana na Ahabu, yote ambayo alifanya, ile nyumba ya pembe aliyojenga, na miji yote aliyojenga, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
40Kwa hiyo Ahabu akalala pamoja na mababu zake, na Ahaziya mwanae akawa mfalme mahali pake.
41Kisha Yehoshafati mwana wa Asa alianza kutawala juu ya Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli.
42Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano alipoanza kutawala, na akatawala Yerusalemu kwa miaka ishirini na mitano. Mama yake alikuwa Azuba, binti wa Shilhi.
43Akatembea katika njia za Asa, baba yake, hakuziacha; akafanya yaliyokuwa mema mbele ya macho ya BWANA. Lakini bado mahali pa juu palikuwa hapajabomolewa. Watu walikuwa bado wanaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba mahali pa juu.
44Yehoshafati akafanya amani na mfalme wa Israeli.
45Kwa mambo mengine kuhusiana na Yehoshafati, na nguvu zake alizoonyesha, na jinsi alivyopigana vita, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
46Aliwaondoa kutoka katka nchi wale makahaba wa kipagani waliokuwa wamebaki katika siku za baba yake Asa.
47Hapakuwepo mfalme katika Edomu isipokuwa kaimu mtawala.
48Yehoshafati alijenga merikebu: ziende Tarshishi na Ofri kuleta dhahabu, lakini hazikusafiri kwa sababu zile merikebu zilivunjika kule Esioni Geberi. Kisha
49Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Naomba watumishi wangu waende pamoja na watumishi wako merikebuni. “Lakini Yehoshafati hakuruhusu hilo.
50Yehoshafati akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi, babu yake; Yoramu mwanawe akawa mfalme mahali pake.
51Ahazia mwana Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli ya Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa mfalme Yehoshafati mfalme wa Yuda, na akatawala kwa mika miwili juu ya Israeli.
52Naye akafanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA akatembea katika njia za baba yake, katika njia za mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwazo aliifanya Israeli kufanya dhambi.
53Alimtumikia Baali na kumwabudu na kwa hiyo akamghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, katika hasira, kama vile baba yake alivyofanya.

Read 1Wafalme 221Wafalme 22
Compare 1Wafalme 22:33-531Wafalme 22:33-53