Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 22

1Wafalme 22:22-41

Help us?
Click on verse(s) to share them!
22Yule pepo akamjibu, 'Nitakwenda na kuwa roho idanganyayo katika vinywa vya manabii wake,' BWANA akamjibu, 'utaweza kumdanganya, na utafanikiwa. Nenda sasa ukafanye hivyo.'
23Tazama sasa, BWANA ameweka roho idangayo kwenye vinywa vya hawa manabii wako, na BWANA ametangaza janga kwako.”
24Kisha Sedekia mwana wa Kenaana, akaja, akamzabua Makaya shavuni, akasema, “Je, yule roho wa Bwana alitokaje kwangu ili asema na wewe?”
25Makaya akasema, “Tazama, “utatambua hilo katika siku hiyo, utakapokimbilia katika chumba cha ndani kujificha.”
26Mfalme wa Israeli akamwambia mtumishi wake, “Mkamate Makaya umpeleke kwa Amoni, liwali wa mji, na kwa mwanangu, Yoashi.
27Mwambie, 'mfalme anasema mweke huyo gerezani na awe anampa mkate kidogo na maji kidogo, mpaka nitakaporudi salama.'”
28Naye Makaya akasema, “Kama utarudi salama basi BWANA hajasema kupitia kinywa changu.” Na akaongeza, “Sikilizeni hili, ninyi watu.”
29Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati mfalme wa Yuda, wamepanda Ramothi Gileadi.
30Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe niende vitani, lakini wewe uvae vazi lako la kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na akaenda vitani.
31Naye mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru majemedari thelathini na mbili wa magari yake, akisema, “Msimwamgamize askari wa muhimu au ambaye si wa muhimu, badala yake mshambulieni mfalme wa Israeli tu.”
32Ikawa wakati majemedari wa magari walipomwona Yehoshafati wakasema, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Wakageuka ili kumshambulia, kwahiyo Yehoshafati akapiga kelele.
33Ikawa majemedari wa magari walipoona kuwa yeye hakuwa mfalme wa Israeli, wakamwacha.
34Lakini mtu mmoja akavuta upinde wake kwa kubahatisha na akampiga mfalme wa Israeli katikati ya mwunganiko wa mavazi yake ya chuma. Ahabu akamawambia dereva wa gari lake, “geuza unirudishe kutoka vitani, kwa kuwa nimeumizwa sana.”
35Vita ikawa mbaya sana siku hiyo na mfalme akalazwazwa garini mwake akiwakabili Washami. Akafa jioni hiyo. Damu ilimwagika kutoka kwenye jeraha lake ndani ya gari.
36Ikawa wakati wa kuzama jua, kilio kikatawala kwa jeshi lote, wakisema, “Kila mtu arudi kwenye mji wake; na kila mtu arudi kwenye mkoa wake!”
37Kwa hiyo mfalme Ahabu akafa na akaletwa Samaria, wakamzika huko Samaria.
38Wakaliosha lile gari kwenye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake (hapa ni mahali ambapo makahaba waliogea), kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limesema.
39Kwa mambo mengine yanayohusisana na Ahabu, yote ambayo alifanya, ile nyumba ya pembe aliyojenga, na miji yote aliyojenga, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
40Kwa hiyo Ahabu akalala pamoja na mababu zake, na Ahaziya mwanae akawa mfalme mahali pake.
41Kisha Yehoshafati mwana wa Asa alianza kutawala juu ya Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli.

Read 1Wafalme 221Wafalme 22
Compare 1Wafalme 22:22-411Wafalme 22:22-41