Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 22

1Wafalme 22:14-50

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Makaya akajibu, “Kama BWANA aishivyo, kile BWANA atakachosema kwangu ndicho nitakachosema.'”
15Naye alipokuja kwa mfalme, mfalme akamwambia, “Makaya, je twende Ramothi Gileadi kupigana, au tusiende?” Makaya akamjibu, “Ivamie na ushinde. BWANA ataitoa kwenye mkono wa mfalme.”
16Kisha mfalme akamwambia. “Je, nikutake mara ngapi ili kuniapia ukweli kwa jna la BWANA?”
17Makaya akasema, “Ninaiona Israeli yote imesambaa kwenye milima, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji, na BWANA amesema, 'Hawa hawana mchungaji. Kila mtu na arudi nyumbani kwake kwa amani.'”
18Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Je sikukwambia kuwa huwa hanitabirii mambo mema yanayonihusu, ila majanga tu?”
19Kisha Makaya akasema, “Kwa hiyo sikiliza neno la BWANA: Nimemwona BWANA akiwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikuwa yamesimama karibu yake upande wake wa kulia na upande wake wa kushoto.
20BWANA akasema, 'Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili kwamba apande akafie Ramothi Gileadi? Na mtu mmoja akajibu kwa njia hii, na mwingine akajbu kwa njia ile.
21Ndipo pepo moja akajitokeza, akasimama mbele ya BWANA, akasema, 'Mimi nitamdanganya.' BWANA akmwuliza, 'Kwa jinsi gani?'
22Yule pepo akamjibu, 'Nitakwenda na kuwa roho idanganyayo katika vinywa vya manabii wake,' BWANA akamjibu, 'utaweza kumdanganya, na utafanikiwa. Nenda sasa ukafanye hivyo.'
23Tazama sasa, BWANA ameweka roho idangayo kwenye vinywa vya hawa manabii wako, na BWANA ametangaza janga kwako.”
24Kisha Sedekia mwana wa Kenaana, akaja, akamzabua Makaya shavuni, akasema, “Je, yule roho wa Bwana alitokaje kwangu ili asema na wewe?”
25Makaya akasema, “Tazama, “utatambua hilo katika siku hiyo, utakapokimbilia katika chumba cha ndani kujificha.”
26Mfalme wa Israeli akamwambia mtumishi wake, “Mkamate Makaya umpeleke kwa Amoni, liwali wa mji, na kwa mwanangu, Yoashi.
27Mwambie, 'mfalme anasema mweke huyo gerezani na awe anampa mkate kidogo na maji kidogo, mpaka nitakaporudi salama.'”
28Naye Makaya akasema, “Kama utarudi salama basi BWANA hajasema kupitia kinywa changu.” Na akaongeza, “Sikilizeni hili, ninyi watu.”
29Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati mfalme wa Yuda, wamepanda Ramothi Gileadi.
30Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe niende vitani, lakini wewe uvae vazi lako la kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na akaenda vitani.
31Naye mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru majemedari thelathini na mbili wa magari yake, akisema, “Msimwamgamize askari wa muhimu au ambaye si wa muhimu, badala yake mshambulieni mfalme wa Israeli tu.”
32Ikawa wakati majemedari wa magari walipomwona Yehoshafati wakasema, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Wakageuka ili kumshambulia, kwahiyo Yehoshafati akapiga kelele.
33Ikawa majemedari wa magari walipoona kuwa yeye hakuwa mfalme wa Israeli, wakamwacha.
34Lakini mtu mmoja akavuta upinde wake kwa kubahatisha na akampiga mfalme wa Israeli katikati ya mwunganiko wa mavazi yake ya chuma. Ahabu akamawambia dereva wa gari lake, “geuza unirudishe kutoka vitani, kwa kuwa nimeumizwa sana.”
35Vita ikawa mbaya sana siku hiyo na mfalme akalazwazwa garini mwake akiwakabili Washami. Akafa jioni hiyo. Damu ilimwagika kutoka kwenye jeraha lake ndani ya gari.
36Ikawa wakati wa kuzama jua, kilio kikatawala kwa jeshi lote, wakisema, “Kila mtu arudi kwenye mji wake; na kila mtu arudi kwenye mkoa wake!”
37Kwa hiyo mfalme Ahabu akafa na akaletwa Samaria, wakamzika huko Samaria.
38Wakaliosha lile gari kwenye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake (hapa ni mahali ambapo makahaba waliogea), kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limesema.
39Kwa mambo mengine yanayohusisana na Ahabu, yote ambayo alifanya, ile nyumba ya pembe aliyojenga, na miji yote aliyojenga, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
40Kwa hiyo Ahabu akalala pamoja na mababu zake, na Ahaziya mwanae akawa mfalme mahali pake.
41Kisha Yehoshafati mwana wa Asa alianza kutawala juu ya Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli.
42Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano alipoanza kutawala, na akatawala Yerusalemu kwa miaka ishirini na mitano. Mama yake alikuwa Azuba, binti wa Shilhi.
43Akatembea katika njia za Asa, baba yake, hakuziacha; akafanya yaliyokuwa mema mbele ya macho ya BWANA. Lakini bado mahali pa juu palikuwa hapajabomolewa. Watu walikuwa bado wanaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba mahali pa juu.
44Yehoshafati akafanya amani na mfalme wa Israeli.
45Kwa mambo mengine kuhusiana na Yehoshafati, na nguvu zake alizoonyesha, na jinsi alivyopigana vita, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
46Aliwaondoa kutoka katka nchi wale makahaba wa kipagani waliokuwa wamebaki katika siku za baba yake Asa.
47Hapakuwepo mfalme katika Edomu isipokuwa kaimu mtawala.
48Yehoshafati alijenga merikebu: ziende Tarshishi na Ofri kuleta dhahabu, lakini hazikusafiri kwa sababu zile merikebu zilivunjika kule Esioni Geberi. Kisha
49Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Naomba watumishi wangu waende pamoja na watumishi wako merikebuni. “Lakini Yehoshafati hakuruhusu hilo.
50Yehoshafati akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi, babu yake; Yoramu mwanawe akawa mfalme mahali pake.

Read 1Wafalme 221Wafalme 22
Compare 1Wafalme 22:14-501Wafalme 22:14-50