Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 20

1Wafalme 20:23-36

Help us?
Click on verse(s) to share them!
23Wale watumishi wa mfalme wa Shamu wakamwambia, “Mungu wao ni mungu wa milimani. Hiyo ndiyo sababu walikuwa na nguvu kuliko tulivyokuwa. Lakini sasa hebu tupigane nao katika nchi tambarare, na kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko wao.
24Na ufanye hivi: waondoe wafalme; mwondoe kila mmoja mahali pake ukaweke majemedari mahali pao.
25Kisha ujihesabie jeshi kama lile jeshi ulilopoteza, farasi kwa farasi na gari kwa gari, nasi tutapigana nao katika nchi tambarare. Kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko walivyo.” Kwa hiyo Beni Hadadi akausikiliza ushauri huo naye akafanya kama alivyoshauriwa.
26Baada ya mwanzo wa mwaka mpya, Beni Hadadi akawahesabu Washami na akapanda Afeki kupigana na Israeli.
27Watu wa Israeli walikuwa wamehesabiwa na walikuwa wamejipanga kupigana nao. Watu wa Israeli wakafanya kambi mbele yao kama makundi mawili madogo ya mbuzi, lakini Washami wakaujaza upande wa nchi.
28Ndipo mtu wa Mungu akaja karibu akaongea mfalme wa Israeli akamwambia, “BWANA anasema: 'Kwa kuwa Washami wamesema kuwa BWANA ni mungu wa milima, na wala si mungu wa mabondeni, nitaliweka hili jeshi kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ni BWANA.'”
29Kwa hiyo majeshi yakaweka kambi yakikabiliana kwa muda wa siku saba. Kisha siku ya saba vita vikaanza. Watu wa Israeli wakawaua Washami 100, 000 wanajeshi wa ardhini kwa siku moja.
30Waliobaki wakakimbilia Afeki, mjini, na ule ukuta ukaanguka juu ya watu ishiriinina saba elfu waliobaki. Naye Beni Hadadi akakimbilia mjini. akaingia kwenye chumba cha ndani.
31Wale watumishi wa Beni Hadadi wakamwambia, “Tazama sasa, tumesikia kwamba wale wafalme wa nyumba ya Israeli ni wenye rehema. Tafadhali hebu tuvaeni magaunia viunoni mwetu na kamba vichwani mwetu, na twendeni kwa mfalme wa Israeli. Labda atakuokoa roho yako.”
32Kwa hiyo wakavaa magunia viunoni mwao na kujifunga kamba vichwani mwao na kisha wakaenda kwa mfalme wa Israeli wakamwambia, “Mtumishi wako Beni Hadadi, anasema, 'tafadhali niachie uhai wangu.” Ahabu akawaambia, “Je, bado yuko hai? Yeye ni ndugu yangu.”
33Sasa wale watu walikuwa wakisikiliza ishara yeyote kutoka kwa Ahabu, kwa hiyo wakamjibu haraka, “Ndiyo ndugu yako Beni Hadadi bado yuko hai.” Ahabu akawaambia, “Nendeni mkamlete.” Ndipo Beni Hadadi alipokuja kwake, na Ahabu akamwacha aje kwenye gari lake.
34Beni Hadadi akamwambia Ahabu, “Nitakurudishia miji yako ambayo baba yangu alichukua toka kwa baba yako, na unaweza kutengeneza masoko kwa ajili yako Dameski, kama baba yangu alivyofanya kule Samaria.” Ahabu akajibu, “Nitakuacha uende kwa agano hili.” Kwa hiyo Ahabu akafanya agano naye kisha akamwacha aende.
35Mtu mmoja, mmoja wana wa wana wa manabii, akamwambia mmoja wa wale manabii wenzake kwa neno la BWANA, “Tafadhali nipige.” Lakini yule mtu akakataa kumpiga.
36Kisha yule nabii akamwambia nabii mwenzake, “Kwa sababu umekataa kutii sauti ya BWANA, mara tu utakaponiacha, simba atakuua.” na mara tu baad ya yule mtu kumwacha, simba akamkuta na kumwua.

Read 1Wafalme 201Wafalme 20
Compare 1Wafalme 20:23-361Wafalme 20:23-36